Je, umeshatumia app ya FaceApp? Hadi sasa utakuwa umekutana na picha za wazee kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii. Lakini tofauti ni kwamba hizi ni picha za watu ambao si wazee kwa sasa.

App ya FaceApp imekuwepo kwa muda mrefu ila imepata umaarufu mkubwa wiki hii. Matokeo ya umaarufu huu umechangiwa na utumiaji wa app hiyo na watu wa aina mbalimbali hii ikiwa ni pamoja na watu maarufu kama vile waigizaji filamu na wanamichezo.

Umaarufu huu umeleta skendo inayohusisha suala la usalama wa data. Vyombo vya habari mbalimbali vimeripoti vikisema app hiyo ambayo inamilikiwa na kampuni ya Urusi inachukua data za maelfu ya picha zinazotokana na utumiaji wa app hiyo. Makao makuu ya kampuni inayomiliki app hiyo yapo katika jiji la Saint-Petersburg nchini Urusi.

Kiukweli hili limekuzwa zaidi na vyombo vya habari za mataifa ya magharibi ambapo chochote chenye historia ya kuwa cha Urusi huwa kinapewa kesi yenye sifa ya kiujasusi. Kiukweli chochote ambacho app hiyo inaweza kufanya na data unazozipatia hasa hasa apa ikiwa ni picha tayari kinaweza fanywa na app zingine maarufu za mataifa ya magharibi kama vile Instagram, Facebook na zingine nyingi.

Tayari kampuni hiyo imeshatoa maelezo ikisema ingawa makao makuu ya app hiyo ni Urusi ila servers zinazotumika katika kupokea na kutengeneza picha mpya hazipo nchini Urusi. Pia si kweli ya kwamba wanahifadhi picha za watu kwa muda mrefu.

Mtafiti wa masuala ya usalama kutoka Ufaransa anayekwenda kwa jina la Elliot Alderson mtandaoni alifanya uchunguzi wa kina na akaja matokeo haya;

  • App hiyo haichukui picha yeyote zaidi ya ile unayotumia kubadili muonekano
  • Pia kuhusu wizi wa data mtafiti huyo amesema pia data pekee zinazochukuliwa ni kitambulisho cha kifaa (device ID) na jina la aina ya simu ambayo imetumika.

Kelele kubwa zinazohusisha udukuzi na wizi wa data hazijapata uthibitisho wowote, na ni jambo linalochukuliwa kwa mtazamo wa kisiasa ambapo vitu vyenye makazi Urusi vinachukuliwa kihofu mara zote.

CHANZO : BBC SWAHILI

Leave a comment