TECHNOLOGY

Apple launches repair program for iPhone 7 users with ‘No Service’ issues — 9to5Mac

Apple today has launched an official repair program for a small number of users experiencing an issue where their iPhone says “No Service”. This issue seems to be specific to the iPhone 7, according to Apple. more…

via Apple launches repair program for iPhone 7 users with ‘No Service’ issues — 9to5Mac

 

Advertisements
Computer, Laptop, Maujanja, TECHNOLOGY

Njia za Kupunguza Mwanga wa Laptop Yako – TeknoKona Teknolojia Tanzania

Je unafahamu njia gani za kupunguza mwanga wa laptop yako? Fahamu njia tatu leo

Source: Njia za Kupunguza Mwanga wa Laptop Yako – TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android, Mobile, MOBILE SAFETY, TECHNOLOGY

Usalama wa nywila kwenye simu yako unatokana na ushikaji wa simu

Neno siri/nywila imekuwa ni kitu ambacho kimezoeleka na pengine mtumiaji kuhisi yuko salama lakini ushikaji wa simu unaweza ukamfanya mtu akajua password

Source: Usalama wa nywila kwenye simu yako unatokana na ushikaji wa simu

Android, Applications, Mobile, MOBILE SAFETY, TECHNOLOGY

USALAMA WA ANDROID YAKO

Google Play store wanakupa nafasi ya kupata Ulinzi wa simu yako ya Android kwa kukuwekea ulinzi wa #AndroidOreo hambayo hulinda simu isishambuliwe na Malware wakati wote.

Android Oreo ni salama kwani ushambulia maadui, hii ni kama kinga ya mwili au chembe nyeupe za damu zinavyoshambulia magonjwa nyemelezi wakati wote.

Android Oreo inavipa viganja vya mikono yako Amani siku zote.

#AndroidOreo 8.0

#Androids

#Googleplay

#Smartphones

ANDROID
Usisahau kushare na wengine katika mitandao ya kijamii, chagua mmoja hapo chini na wengine waone.

EXECUTIVE EDITOR

Android, Applications, Maujanja, TECHNOLOGY

Jinsi ya Ku-Install Windows mbalimbali kwenye Simu za Android (Windows 10, XP,W8)

Natumai hujambo mdau wa Kaguttatech, Leo nimekuletea #Maujanja jinsi ya kuinstall Windows mbalimbali kwenye simu za Androids.

Kuna wakati unaboreka kutumia simu yako katika mfumo wa kawaida, hasa mpangilio wa #Applications zako na #Menu ya simu yako.

Hapa nimekuletea namna na jinsi ya kuinstall Applications (Windows) kama utumiavyo Kompyuta yako.

Kumbuka: Njia zote hizi hazihitaji ku-root simu yako!

Fuata link zifuatazo ili kupata Windows tofauti tofauti.

Chagua Windows Mojawapo kati ya hizi huifurahie simu yako. Usisite kunitafuta kwa msaada zaidi.

1. NEW UPDATE 2017

2. LIMBO INSTALLATION

3. ANDROIDS WINDOWS 
4. WINDOWS 10

Kwa msaada:

FACEBOOK
Kumbuka kisambaza (Share) na wengine waone.

Android, Applications, Maujanja, Mobile, TECHNOLOGY, WhatsApp

Jinsi ya kuunganisha Simu yako itumie Keyboard na Mouse.

Umechoka kushika Simu na kuandika ujumbe mrefu au habari ndefu? Nimekuletea njia rahisi ya kuunganisha Simu yako ili itumie Keyboard Pamoja na Mouse kwa Urahisi.

Tizama VIDEO niliyokuwekea hapa ili kuweza kupata hatua za kufuata. Usisahau kusambaza ili wengine waone pia, usiwe mchoyo siku zote.

Toa maoni pia ili nijue kama kutakuwa na tatizo au mafanikio.

BOFYA HAPA

TECHNOLOGY

Jifunze jinsi ya kutumia Code ya US(+1) kwenye namba yako ya WhatsApp

Umewahi kujiuliza ni kwa namna gani watu wapo katika nchi zao lakini bado wanatumia namba za nje ya nchi Fulani katika WhatsApp?

  • Nimekuwekea hatua zote za kufuata ili kubadili namba yako ya WhatsApp ili itukie CODE Ya US kwa urahisi.

BOFYA HAPA KUTAZAMA

Kumbuka Kusambaza ili wengine waone pia, usisite kuniwekea maoni yako hapa.

TECHNOLOGY

Njia 3 Za Ku ‘Reset’ Simu Ya Android!


Inafahamika wazi kuwa simu za Android kama vile Samsung Galaxy ndio wapinzani wakubwa wa kampuni Ya Apple ambao wana iPhone zinazotumia iOs. Watu wengi wanasema simu za android ni rahisi kutumia kuliko zile za Apple, Mimi nasema inategemea na mtu na chaguo lake (ha!). Watumiaji wa Android wanafurahia maelfu kwa maelfu ya aplikesheni (Application) zinazopatikana bureGoogle play.

Lakini kushusha aplikesheni nyingi katika simu yako inashusha kasi ya ufanyaji kazi wa simu yako, Je hili likitokea unafanyaje?. ikitokea hivi ni vizuri kureset simu yako, Lakini pia kureset simu yako kuna kanuni zake na zisipofuatwa unaweza jikuta unaharibu kifaa (simu) chako. Twende wote sambamba kuzijua njia tatu za kureset simu au tableti yako ya Android

Jinsi Ya Kureset Simu/Tableti  Ya Android
Kabla ya kufuata maelezo haya kureset kutafuta Data zako zote zilizo kwenye simu (number za simu,miziki,picha,notes,mafil ulioshusha kutoka GooglePlay n.k). Hivyo basi unashauriwa kufanya back up ya data zako kwanza. Kisha Toa laini na Memori Kadi katika simu Hiyo ya Android Pia inashauriwa charge iwe angalau asilimia hamsini (50%).
1. Kureset Kwa Kutumia Factory Reset

Hi ni njia rahisi kabisa ya kureset simu yako. kinachotakiwa ni kwenda kwenye Menu ya simu yako kisha unaenda kwenye Settings kisha unabofya Backup And Restore baada ya hapo unaenda kwenye Factory Reset. Kitu cha muhimu kujua hapa ni kwamba ukifanya hivi vitu vyako vitafutika hivyo ni muhimu kufanya back up ya data zako zote kabla hujafanya hivi.

2. Kureset Kwa Kutumia USSD kodikuna baadhi ya simu facory reset haipatikani kama ilivyoelekezwa hapo juu, nenda kwenye Privacy Settings

Watengenezaji wa simu wengi kama Samsung, HTC n.k huwa wanatoa kodi inayoweza ku ‘restore’ simu ya Android. Kodi hiyo ni *#7780#

kwa hiyo kila utakapo piga hiyo kodi simu yako ya adroid itakuuliza kufomati. Ni vizuri kuback up data zako pia kwa sababu baadhi ya simu haziulizi ukipiga tuu hiyo kodi simu inaanza kufomati.

3. Kureset Kwa Kutumia System Restore

Hi njia ya mwisho ni ngumu kidogo na haifahamiki sana laki ndio njia yenye nguvu kuliko hizo mbili hapo juu. Sifa za njia hii ni kwamba inafanya kazi hata simu yako ikiwa imeji ‘lock’ (kama umesahau pattern au password ya simu yako). Njia (1 na 2) hazitafanya kazi kama simu yako itakua imeji ‘loki’.

JINSI

A. Zima Simu Yako Ya Android

  • Kama ni Mtumiaji Wa Samsung Bonyeza: Sauti juu + Home + Kuzima. Mara baada ya simu kunguruma achia kitufe cha kuzima. Mara simu ikiwa katika modi ya ‘Recovery’ achia kitufe cha sauti juu na cha home pia
  • Kama Ni Mtumiaji Wa HTC Bonyeza: Sauti Chini + Kuzima. Simu ikiwa inawaka achia kitufe cha kuwasha, ukiona imetokea modi ya ‘Recovery’ achia kitufe cha Sauti Chini
  • Kama Ni Mtumiaji Wa Micromax Bonyeza: Sauti Juu + Kuzima

B. Ukishaingia katika menyu ya System Restore tumia kitufe cha Sauti Juu Na Sauti Chini Kuchagua chaguo lako na kitufe cha kuwasha/kuzima simu kuchagua chaguo hilo

C. Sasa chagua chaguo lako kureset simu yako ya Android

Hii njia itachukua mda kidogo katika ufanyaji kazi wake laki unashauriwa kutotoa betri ya simu yako maana italeta hitilafu wakati wa kureset . Naimani njia hizi tatu zitakusaidia sana kureset simu yako mwenyewe bila kuwapelekea mafundi au wataalamu wowote maana utaingia gharama. Kwa nini ulipie kazi ambayo unaweza ifanya mwenyewe?

Unamawazo yoyote kuhusu hiki nilichokupatia kwa Leo? Usisite kuniandikia maoni yako sehemu ya hapo chini utakuwa umefanya vyema zaidi.

Android

WhatsApp yaongeza aina za herufi na rangi katika Status kwa matoleo ya Android na iOS

Toleo jipya la WhatsApp laanza kupatikana. WhatsApp imetangaza kufanya maboresho ya programu yake pendwa kwa kuweka kipengele kipya ambacho kitamuwezesha mtumiaji wake kutumia aina ya Fonts(herufi) mbalimbali azitakazo.
Kipengele hicho kipya kitakuwa katika sehemu ya kuweka Status ambapo mtumiaji ataweza kuweka background ya rangi yoyote aipendayo na kisha kuandika chochote akipendacho kwa aina ya muandiko aupendao.

Aina ya herufi za namna tano kwa sasa ndio pekee zinazopatikana pamoja na rangi 22.

Kwa mujibu wa WhatsApp maboresho haya yanapatikana kwa matoleo yote ya Android na iOS. Ili kupata mabadiliko hayo ni lazima ufanye Update kwa WhatsApp yako.

  • Kuwezesha zoezi hilo, kwanza fungua whatsApp yako, angalia juu na ufungue Status.
  • Ukishafungua kwa chini upande wa kulia utaona kama alama ya kalamu na utaifungua.

Hapo utakuwa umeingia kwenye uwanja wa kuandika Status yako na kuchagua muandiko uupendao na rangi za Background uzipendazo. Maboresho haya yanafanana na yale ya Facebook.
Pia kwa wale wanaotumia WhatsApp Web (kwenye kompyuta) kwa sasa wataweza badilisha Status moja kwa moja.

Kumbuka kila baada ya masaa 24 Status itajiondoa na hivyo kulazimika kuiweka tena au kuweka mpya.

Kwa ushauri usisite kunitafuta kupitia:

FACEBOOK
KAGUTTA TECH. THE HOME EXPERTS