Njia 3 Za Ku ‘Reset’ Simu Ya Android!


Inafahamika wazi kuwa simu za Android kama vile Samsung Galaxy ndio wapinzani wakubwa wa kampuni Ya Apple ambao wana iPhone zinazotumia iOs. Watu wengi wanasema simu za android ni rahisi kutumia kuliko zile za Apple, Mimi nasema inategemea na mtu na chaguo lake (ha!). Watumiaji wa Android wanafurahia maelfu kwa maelfu ya aplikesheni (Application) zinazopatikana bureGoogle play.

Lakini kushusha aplikesheni nyingi katika simu yako inashusha kasi ya ufanyaji kazi wa simu yako, Je hili likitokea unafanyaje?. ikitokea hivi ni vizuri kureset simu yako, Lakini pia kureset simu yako kuna kanuni zake na zisipofuatwa unaweza jikuta unaharibu kifaa (simu) chako. Twende wote sambamba kuzijua njia tatu za kureset simu au tableti yako ya Android

Jinsi Ya Kureset Simu/Tableti  Ya Android
Kabla ya kufuata maelezo haya kureset kutafuta Data zako zote zilizo kwenye simu (number za simu,miziki,picha,notes,mafil ulioshusha kutoka GooglePlay n.k). Hivyo basi unashauriwa kufanya back up ya data zako kwanza. Kisha Toa laini na Memori Kadi katika simu Hiyo ya Android Pia inashauriwa charge iwe angalau asilimia hamsini (50%).
1. Kureset Kwa Kutumia Factory Reset

Hi ni njia rahisi kabisa ya kureset simu yako. kinachotakiwa ni kwenda kwenye Menu ya simu yako kisha unaenda kwenye Settings kisha unabofya Backup And Restore baada ya hapo unaenda kwenye Factory Reset. Kitu cha muhimu kujua hapa ni kwamba ukifanya hivi vitu vyako vitafutika hivyo ni muhimu kufanya back up ya data zako zote kabla hujafanya hivi.

2. Kureset Kwa Kutumia USSD kodikuna baadhi ya simu facory reset haipatikani kama ilivyoelekezwa hapo juu, nenda kwenye Privacy Settings

Watengenezaji wa simu wengi kama Samsung, HTC n.k huwa wanatoa kodi inayoweza ku ‘restore’ simu ya Android. Kodi hiyo ni *#7780#

kwa hiyo kila utakapo piga hiyo kodi simu yako ya adroid itakuuliza kufomati. Ni vizuri kuback up data zako pia kwa sababu baadhi ya simu haziulizi ukipiga tuu hiyo kodi simu inaanza kufomati.

3. Kureset Kwa Kutumia System Restore

Hi njia ya mwisho ni ngumu kidogo na haifahamiki sana laki ndio njia yenye nguvu kuliko hizo mbili hapo juu. Sifa za njia hii ni kwamba inafanya kazi hata simu yako ikiwa imeji ‘lock’ (kama umesahau pattern au password ya simu yako). Njia (1 na 2) hazitafanya kazi kama simu yako itakua imeji ‘loki’.

JINSI

A. Zima Simu Yako Ya Android

  • Kama ni Mtumiaji Wa Samsung Bonyeza: Sauti juu + Home + Kuzima. Mara baada ya simu kunguruma achia kitufe cha kuzima. Mara simu ikiwa katika modi ya ‘Recovery’ achia kitufe cha sauti juu na cha home pia
  • Kama Ni Mtumiaji Wa HTC Bonyeza: Sauti Chini + Kuzima. Simu ikiwa inawaka achia kitufe cha kuwasha, ukiona imetokea modi ya ‘Recovery’ achia kitufe cha Sauti Chini
  • Kama Ni Mtumiaji Wa Micromax Bonyeza: Sauti Juu + Kuzima

B. Ukishaingia katika menyu ya System Restore tumia kitufe cha Sauti Juu Na Sauti Chini Kuchagua chaguo lako na kitufe cha kuwasha/kuzima simu kuchagua chaguo hilo

C. Sasa chagua chaguo lako kureset simu yako ya Android

Hii njia itachukua mda kidogo katika ufanyaji kazi wake laki unashauriwa kutotoa betri ya simu yako maana italeta hitilafu wakati wa kureset . Naimani njia hizi tatu zitakusaidia sana kureset simu yako mwenyewe bila kuwapelekea mafundi au wataalamu wowote maana utaingia gharama. Kwa nini ulipie kazi ambayo unaweza ifanya mwenyewe?

Unamawazo yoyote kuhusu hiki nilichokupatia kwa Leo? Usisite kuniandikia maoni yako sehemu ya hapo chini utakuwa umefanya vyema zaidi.

WhatsApp yaongeza aina za herufi na rangi katika Status kwa matoleo ya Android na iOS

Toleo jipya la WhatsApp laanza kupatikana. WhatsApp imetangaza kufanya maboresho ya programu yake pendwa kwa kuweka kipengele kipya ambacho kitamuwezesha mtumiaji wake kutumia aina ya Fonts(herufi) mbalimbali azitakazo.
Kipengele hicho kipya kitakuwa katika sehemu ya kuweka Status ambapo mtumiaji ataweza kuweka background ya rangi yoyote aipendayo na kisha kuandika chochote akipendacho kwa aina ya muandiko aupendao.

Aina ya herufi za namna tano kwa sasa ndio pekee zinazopatikana pamoja na rangi 22.

Kwa mujibu wa WhatsApp maboresho haya yanapatikana kwa matoleo yote ya Android na iOS. Ili kupata mabadiliko hayo ni lazima ufanye Update kwa WhatsApp yako.

  • Kuwezesha zoezi hilo, kwanza fungua whatsApp yako, angalia juu na ufungue Status.
  • Ukishafungua kwa chini upande wa kulia utaona kama alama ya kalamu na utaifungua.

Hapo utakuwa umeingia kwenye uwanja wa kuandika Status yako na kuchagua muandiko uupendao na rangi za Background uzipendazo. Maboresho haya yanafanana na yale ya Facebook.
Pia kwa wale wanaotumia WhatsApp Web (kwenye kompyuta) kwa sasa wataweza badilisha Status moja kwa moja.

Kumbuka kila baada ya masaa 24 Status itajiondoa na hivyo kulazimika kuiweka tena au kuweka mpya.

Kwa ushauri usisite kunitafuta kupitia:

FACEBOOK
KAGUTTA TECH. THE HOME EXPERTS

UTAFITI: Hizi ndio Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi katika simu za Android

​Ikiwa simu yako ya Android haina kasi, wala nafasi ya ziada ya kuongeza programu nyingine ni wakati sasa wa kufuta baadhi programu ili kuondoa matatizo hayo.
Baadhi ya programu za simu za mkononi hutumia kiwango kikubwa cha nafasi na kiwango kikubwa cha matumizi ya Betri na hivyo kuathiri utendaji wa simu yako.

Katika utafiti mpya wa simu za Android zaidi ya milioni tatu uliofanywa, watafiti wametaja orodha ya programu zinazokula sana chaja ya Betri kwa kiwango kikubwa na zile zinazochukua nafasi zaidi katika simu.

Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi: Apps tunazozitumiaga na zinaongeza kwa ulaji wa chaji pale zinapotumika
Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi: Apps tunazozitumiaga na zinaongeza kwa ulaji wa chaji pale zinapotumika

Ripoti hiyo iliyotolewa na Kampuni ya usalama wa kimtandao ya Avast miongoni mwa programu zilizoongoza kwa ulaji wa Betri ni zile za Google wenyewe, kama Google Maps, Google Play Music, Google Plus na Google Hangouts.
Programu hizi huja pamoja na mfumo Endeshi wa Android na hata kama huzitumii hufanya kazi kwa nyuma ya mfumo pale tu simu inapokuwa umeiwasha zenyewe zinatumia data.

Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi : Apps zinazoanza kufanya kazi mara tuu ukiwasha simu yako na zinatumia kiwango kikubwa cha chaji ya betri yako

Aidha pia kuna programu/apps zingine zinazokula Betri kwa kasi ni zile za Samsung kama AllShare, ChatON na Push Service.

Vile vile watafiti hao wamegundua kwamba Google Docs na Text-to-Speech ni miongoni mwa programu zinazoongoza kula Chaji sambamba na Samsung WatchON, Video Editor na Media Hub.

Programu zingine zilizoorodheshwa kula Chaji ni SHAREit, Flipboard, Line na Adobe Acrobat Reader.

Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi: Orodha ya apps ambazo huwa zinafanya simu yako kuwa nzito kiutendaji pale unapozitumia

Wakati Avast wakitoa ripoti ya Programu zinazokula Chaji pia na zile zinazokula nafasi kubwa katika simu yako hazikuachwa nyuma.

  • Programu zilizoorodheshwa kwa kuongoza katika ulaji wa nafasi ni pamoja na WhatsApp, WeChat na Snapchat ambapo zimetajwa kuwa sambamba na zile za Netflix na Spotify.
  • Instagram, Facebook Messenger na Snapchat zimetajwa kula nafasi kubwa sawa na Amazon kindle na BBC News App.
  • Avast iligundua pia vivinjari (Browser) vya Chrome, Firefox na app ya barua pepe ya Microsoft Outlook pia zinakula Data kwa kiwango kikubwa.
Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi : Orodha ya Apps zinafanya kazi mara tuu ukiwasha simu na huwa zinafanya simu yako kuwa nzito zaidi kiutendaji

Gagan Singh makamu wa Rais na Meneja mkuu wa biashara wa Avast amesema kwa maisha ya sasa simu janja zimekuwa ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.

  • Ushauri ambao umetolewa na Avast kwa watumiaji wa Simu za Android kwa wale ambao wanataka kuimarisha utendaji wa simu zao wasisite kuondoa (Kufuta) programu ambazo zinakula chaji ya Betri, nafasi hata kama wanazipenda.

Kampuni ya Avast imependekeza kuzuia Arifa (notifications), kuzuia Programu zinazofanya kazi zenyewe bila ya kufunguliwa.
Aidha imeshauriwa kuimarisha utendaji wa simu kwa kufuta cache mara kwa mara, kufuta data, kuzima Wi-Fi, Bluetooth na GPS pale ambapo huna matumizi nazo. Pia imeshauriwa kupunguza mwanga wa simu katika Skrini yako.

Angalizo baadhi ya programu huwezi kuzifuta mpaka simu ya ko iwe imefanyiwa root hususani zile zinazokuja pamoja na mfumo endeshi wa Android.

Chanzo: WordTechnology.com

Nitembelee FACEBOOK Pia kumbuka Kushare.

Google yaongeza lugha ya kiswahili katika voice search

Kampuni ya Google imetangaza uzinduzi wa lugha 30 za sehemu mbalimbali duniani zitakazoweza kutumika katika kipengele chake cha Voice search na lugha ya kiswahili ikiwemo.


Voice search hutumika katika Android na iOS kumsaidia mtu kuweza kutafuta kitu bila ya kubonyeza au kuandika na badala yake anazungumza kwa lugha ambayo imeorodheshwa na Google.

Lugha zilizoongezwa ni;

  • Amharic (Ethiopia)
  • Armenian (Armenia)
  • Azerbaijani (Azerbaijani)
  • Bengali (Bangladesh, India)
  • English (Ghana, Kenya, Nigeria, Tanzania)
  • Georgian (Georgia)
  • Gujarati (India)
  • Javanese (Indonesia)
  • Kannada (India)
  • Khmer (Cambodian)
  • Lao (Laos)
  • Latvian (Latvia)
  • Malayalam (India)
  • Marathi (India)
  • Nepali (Nepal)
  • Sinhala (Sri Lanka)
  • Sundanese (Indonesia)
  • Swahili (Tanzania, Kenya)
  • Tamil (India, Singapore, Sri Lanka, Malaysia)
  • Telugu (India)
  • Urdu (Pakistan, India)

Kuanzia sasa watumiaji wataweza kutafuta vitu kwa lugha hizo.
Lugha hizo pia zitapatikana katika Google search katika mfumo wa iOS. Kwa mujibu wa Google kutumia sauti kutafuta kitu ni njia ya kasi zaidi ya mara tatu kuliko ile ya kuandika.

Kuongezwa kwa lugha ya kiswahili na Amharic (Ethiopia) ambazo ni lugha maarufu Afrika kumeelezwa kutaongeza watumiaji wa Voice search.

Kwa miaka ya karibuni lugha ya kiswahili imeendelea kupata waongeaji wengi duniani na kuanza kufundishwa katika vyuo vikuu mbalimbali katika nchi kadhaa barani Afrika, Ulaya na Asia.

Kiswahili ni lugha yetu, sasa inakua kwa kasi duniani mpaka kufikia kutumika vyema katika masuala ya Kimtandao. 

Niandikie maoni yako lakini usisahau kushare ili wengine waone.

MAWASILIANO:

FACEBOOK

INSTAGRAM

TWITTER

Mbinu 10 Za Kutumia Intaneti Kwenye Kompyuta!

​Tumia kompyuta yako kama mtaalam/mzoefu, hii itakusaidia katika kumaliza kazi katika muda mchache. Ushawahi kuona wale wanadokoa herufi moja moja? (ha!). Sasa utatumia vipi vizuri muda wako kama uko taratibu na hujui aina mbalimbali ya maujanja na njia za mkato ukiwa mtandaoni/intaneti? Lazima upoteze muda sio?

Nina uhakika kila mtu anapenda njia za mkato na mbinu mbalimbali wakati anapokua anatumia kompyuta yake. Sasa basi zifuatazo ndio njia na mbinu mbalimbali unazoweza tumia ukiwa katika mtandao kwa kompyuta yako.
1. NJIA YA MKATO KWENDA KWENYE WEBSITE

Haina haja ya kuandika sana ili upate kuingia katika mtandao unayoipenda. Kiurahisi andika jina la mtandao unaotaka kuingia bila kuweka ‘www.’ mwanzoni wala ‘.com’ mwiahoni kisha bonyeza CTRL+Enter itakupeleka kwenye tovuti hiyo, Mfano unataka kuingia na kusoma makala za http://www.kaguttatech.wordpress.com basi andika Teknolojiatanzania kisha bonyeza CTRL+Enter kwa mkupuo, mambo yatajipa

2. HIFADHI UKURASA KAMA PDF

Unaweza hifadhi ukurasa unaouhitaji kama PDF lakini hii inatengemea na ‘Browser’ unayoitumia. Ukitumia Google Chrome unaweza ifanya ukurasa kama PDF. Nenda kwenye ukurasa unaoutaka kisha bofya CTRL+P kama unatumia Windows na Cmd+P kama watumia MAC

3. PATA TENA UKURASA ULIOFUNGA/FUTA

Hili linavutia, unaweza pata ukurasa uliofunga kwa bahati mbaya. Kufanya hivyo bonyeza Ctrl + Shift + T ili kuupata tena. Vipi kama ulifunga kurasa mbili tofauti kwa bahati mbaya au hata tatu? basi bonyeza Ctrl + Shift + T mara mbili ili kupata kurasa ya pili na mara tatu kupata kurasa ya tatu na kuendelea.

4. ONYESHA URL KATIKA BROWSER

Unaweza ukaonesha (Highlight) URL katika browser kwa kubofya CTRL + L . na kisha utaamua ufanye nini mfano ukiamua kuinakili hiyo URL utabofya CTRL + C

5. NJIA RAHISI YA KUFUNGUA TASK MANAGER

Imezoeleka kufungua Task Manager kwa kutumia njia hii CTRL+ALT+DEL lakini njia hii si nzuri kwa sababu haikupeleki kwenye Task Manager moja kwa moja, inakupeleka katika menu/mchaguo fulani hivi ndani ya huo mchaguo ndio unaweza chagua Task Manager. Kwa nini upitie yote hayo? Bonyeza CTRL+SHIFT+ESC kuifungua Task Manager moja kwa moja.

6. KUUKUZA UKURASA NJE NA NDANI

Ndio unaweza kuukuza ukurasa nje au ndani (zoom in and Out). Kama haujaridhishwa na ukubwa wa muonekano wa ukurasa wako unaweza kuubadilisha, unaweza kuukuza muenekano huo au kuufanya uwe muonekano mdogo inategemea na wewe unataka nini. Ili kufanya hivyo inakubidi ubofye CTRL+ au CTRL- kisha ukubwa wa ukurasa utabadilika

7. NJIA YA MKATO KWA UKURASA MPYA

Haina haja ya kutumia nguvu njingi kufungua anuani/Link katika ukurasa unaofuata. unaweza fanya hivyo kwa urahisi tuu sogeza kipanya(mouse) yako juu ya LINKI husika kisha bonyeza CTRL na Left. Bofya hapo link itafunguka katika ukurasa mwingine

8.SIMAMISHA KWA MDA VIDEO YOUTUBE

Unaweza ukawa unatumia Space Bar kushusha ukurasa chini na kusimamisha kwa muda (pause) video za Youtube. Lakini unaweza ukatenga kazi hizi mbili. Bonyeza K kusimamisha kwa mda video na bonyeza Space Bar kushuka chini katika ukurasa huo huo mmoja

9. NJIA YA MKATO KWENDA SEHEMU YA DOWNLOADS

Hii haijilishi kama unatumia Mozila Firefox au Google Chrome. Kama unatafuta mafaili ulioshusha au yale unayo shusha bonyeza CTRL + J na utapelekwa kwenye ukurasa huo

10. NJIA YA MKATO YA KUFUTA CACHE

Unaweza ukafuta cache za ‘browser’ yako kwa kubonyeza CTRL+SHFT+R kisha refresh ukurasa huo.

Kuna mbinu kibao na maujanja mengi sana juu nini unaweza fanya na browser ya kompyuta yako. Ningependa kusikia kutoka kwako lipi halipo hapa na unalifahamu…

Kwa MAUJANJA zaidi Bofya TEKNOLOJIA MPYA

Jinsi ya ku-unlock modem na kuweza kutumia sim card yoyote.

​Kutokana na ukuaji wa kasi wa matumizi ya intaneti kumepelekea makapuni ya simu za mikononi kubuni matumizi ya modem kwa ajili ya kuweza kupata huduma ya intaneti.

Ingawa kuna makampuni mengi ya simu na kila kampuni ina modems zake na ushindani pia kuchukua nafasi yake kwa kila kampuni kuwa na huduma ya vifurushi vitakavyowavutia wateja. Suala la kujiuliza ni je, utakuwa na modem kutoka kila kampuni kwa sababu huduma zao zimekuvutia ? Hapana, jambo la kuzingatia ni kuwa na modem moja ambayo itakuwezesha kutumia line yoyote.
Hapa tutakuelekeza kwa kutumia Huawei E173, fuata maelekezo kulingana na aina ya modem yako.

Jinsi ya ku-unlock Huawei E173 modem
 1. Pakua programu wezeshaji iitwayo  Huawei ‘ Mobile Partner ‘ kwa ajili ya Windows OS kama unatumia Windows kwnye kompyuta yako. Baada ya kuopakua ‘right click’ kisha bofya ‘ Run as administrator‘. Kisha fuata maelekezo mpaka mwisho na kuistall.
2. Weka sim card kwenye modem ambayo ni tofauti na kampuni ya simu; kama ni modem ya Airtel weka sim card ya Tigo, Voda, n.k ila sio line ambayo ni kutoka kampuni hiyohiyo inazotoa modem unayotumia kisha subiri mpaka iwe detected. Usiinstall programu (mobile partner) iliyokuja na modem .

3. Pakua na kuinstall DC Unlocker ya hivi karibuni . Kisha ifungue na kuchagua ‘ Huawei ‘ pia, chagua ‘ Auto detect(recomended) ‘ kisha bofya kitufe cha kutafuta(search).

4. Funga mobile partner pamoja na DC Unlocker kisha download Firmware toleo la hivi karibuni. Ondoa mafaili hayo katika mkusanyiko wa pamoja(zip) kisha right click kwenye setup na ifungue kama administrator. Install mpaka mwisho wa mchakato mzima wa installation.

5. Restart DC Unlocker . Kisha ifungue na kuchagua ‘ Huawei ‘ pia, chagua ‘ Auto detect(recomended) ‘ kisha bofya kitufe cha kutafuta(search).

6. Ili kuweza kufungua modem yako inabidi ulipie pesa kidogo kama Tsh 9,000 kwa kutumia Paypal kisha bonyeza severs

kuweza kuweka username na password ambayo utatumiwa kwenye email address yako.

7. Bonyeza ‘ Unlock ‘ kisha chagua ‘ Read Unlock Code and auto enter to modem‘ halafu bonyeza ‘ Do job‘.

8.Bonyeza sehemu ya kutafuta(search) kuhakiki kama modem yako imfunguka na utaona sehemu ya ‘ Sim lock status‘ imeandikwa imefunguliwa (unlocked).

Napatikana katika Account :

Facebook na Instagram

Deal: Galaxy S7 edge on Verizon or Sprint for just $191.76, today only.

Sure, the Galaxy S8+ is official and on sale, and has been for many months now. But that doesn’t mean last year’s Galaxy S7 edge isn’t a good performer even in this day and age. And since it’s older, the deals for it are much better than for its successor.

Case in point: today only, Best Buy is holding a sale on S7 edge units for Verizon and Sprint. You need to become a customer of one of those carriers, or to already be one. If so, you can grab the S7 edge for just $7.99 per month with two-year installments.

That means the grand total you will pay for the device over the course of those 24 months is a staggeringly low $191.76. That’s a far cry from the phone’s initial price, but it’s also much cheaper than you can find it elsewhere today. Do keep in mind however that the deal expires after 11:59 PM CT, so act fast if you’re interested.

For Verizon, your color options are Black Onyx and Silver Titanium, while for Sprint those are joined by Gold Platinum and Blue Coral.

Join the Origin in GSMarena.com