WhatsApp yaongeza aina za herufi na rangi katika Status kwa matoleo ya Android na iOS

Toleo jipya la WhatsApp laanza kupatikana. WhatsApp imetangaza kufanya maboresho ya programu yake pendwa kwa kuweka kipengele kipya ambacho kitamuwezesha mtumiaji wake kutumia aina ya Fonts(herufi) mbalimbali azitakazo.
Kipengele hicho kipya kitakuwa katika sehemu ya kuweka Status ambapo mtumiaji ataweza kuweka background ya rangi yoyote aipendayo na kisha kuandika chochote akipendacho kwa aina ya muandiko aupendao.

Aina ya herufi za namna tano kwa sasa ndio pekee zinazopatikana pamoja na rangi 22.

Kwa mujibu wa WhatsApp maboresho haya yanapatikana kwa matoleo yote ya Android na iOS. Ili kupata mabadiliko hayo ni lazima ufanye Update kwa WhatsApp yako.

  • Kuwezesha zoezi hilo, kwanza fungua whatsApp yako, angalia juu na ufungue Status.
  • Ukishafungua kwa chini upande wa kulia utaona kama alama ya kalamu na utaifungua.

Hapo utakuwa umeingia kwenye uwanja wa kuandika Status yako na kuchagua muandiko uupendao na rangi za Background uzipendazo. Maboresho haya yanafanana na yale ya Facebook.
Pia kwa wale wanaotumia WhatsApp Web (kwenye kompyuta) kwa sasa wataweza badilisha Status moja kwa moja.

Kumbuka kila baada ya masaa 24 Status itajiondoa na hivyo kulazimika kuiweka tena au kuweka mpya.

Kwa ushauri usisite kunitafuta kupitia:

FACEBOOK
KAGUTTA TECH. THE HOME EXPERTS

Leave a comment